TAMASHA LA KITAIFA LA KISWAHILI NA UTAMADUNI KUFANYIKA MS TCDC SEPTEMBA 2019
Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) likishirikia na chuo cha MS TCDC wameandaa Tamasha la kitaifa la Kiswahili na Utamaduni litakalofanyika kwa siku tatu mapema mwezi septemba mwaka huu .Kauli mbiu ya Tamasha hili ni “Tukienzi Kiswahili na Utamaduni kama Nyenzo Muhimu za Maendeleo”. Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Tamasha hili anatarajiwa kua ni waziri wa Habari , Sanaa ,Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe.
Tamasha hili linatazamia kuwaleta pamoja wapenzi na wadau wa lugha ya Kiswahili, vyama vya Kiswahili, waandishi na wachapishaji wa vitabu vya Kiswahili , wanafunzi na waalimu wa Kiswahili , wanafunzi wa kigeni wanaojifunza lugha ya Kiswahili , Taasisi zinazofundisha lugha ya Kiswahili na Utamaduni pamoja na wanahabari kwa siku tatu mfululizo kuanzia Septemba 12 hadi 14 mwaka huu.
Ikiwa lengo kuu ni kukuza Kiswahili na utamaduni , kubadilisha uzoefu, kujadili mambo mbalimbali yanayohusu lugha ya Kiswahili na utamaduni Tamasha hili pia litafungua milango kwa wadau mbalimabali wa Kiswahili pamoja na wafanyabishara wa bidhaa na huduma zinazo husu Kiswahili na tamaduni za kiswahili kuonesha bidhaa zao katika siku tatu za Tamasha.
Tamasha hili linakuja wakati ambapo kikao cha wakuu wanchi za SADC kinamalizika jijini Dar mwanzoni mwa mwezi Agosti ambapo maswala yaliyo afikiwa na viongozi hao ni pamoja na kukifanya Kiswahili kua lugha rasmi ya umoja huo uliopo chini ya Mwenyekiti wa sasa Mh. Dkt John Pombe Magufuli ambaye ameonesha nia ya kukipeleka Kiswahili nje ya mipaka ya Afrika Mashariki.
Kwa maelezo zaidi juu ya namna ya kushiriki au kuwa mmoja wa wanamanesho wasiliana nasi kwa simu namba 0713 727 806 / 0754 651 715 au kwa barua pepe tamasha2019@mstcdc.or.tz au tembelea wavuti ya tamasha https://sikuyakiswahili.org