Upangaji na Usimamizi wa Miradi ya Maendeleo Level II
Je, wewe ni msimamizi au meneja au mratibu au afisa kwenye mradi wa maendeleo? Mafunzo haya ya Upangaji na Usimamizi wa Miradi ya Maendeleo yatakuwezesha kuelewa mzunguko mzima katika kupanga, kutekeleza na kusimamia shughuli zote za mradi wowote wa maendeleo – kuanzia uibuaji wa changamoto zinazoikabili jamii, kupanga shughuli zitakazojikita katika kutatua changamoto hizo, kufuatilia utekelezaji wa shughuli hizo na kuratibu shughuli za mradi mzima.
*Mafunzo haya yana hatua mbili. Hatua ya kwanza hujikita zaidi kwenye upangaji na utekelezaji wa mradi wa maendeleo wakati hatua ya pili hujikita zaidi kwenye ufuatiliaji na uratibu wa mradi wa maendeleo.
Hatua ya kwanza: 15 – 19 Machi 2021
Hatua ya pili: 22 – 26 Machi 2021
Hatua ya kwanza: 21 – 25 Juni 2021
Hatua ya pili: 28 Juni – 2 Julai
Hatua ya kwanza: 18 – 22 Octoba 2021
Hatua ya pili: 25 – 29 Octoba 2021
$295